94. Du´aa ya kuchelea mkosi

  Download

205-

اللّهُـمَّ لا طَيْـرَ إِلاّ طَيْـرُك، وَلا خَـيْرَ إِلاّ خَـيْرُك، وَلا إِلهَ غَيْـرُك

”Ee Allaah! Hapana mkosi isipokuwa ulioukadiria Wewe, hapana kheri isipokuwa kheri Yako na hapana mungu wa haki asiyekuwa Wewe.”[1]

[1] Ahmad (02/220) na Ibn-us-Sunniy (292). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “al-Ahaadiyth adh-Dhwa´iyfah” (03/54). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akipendezewa na al-Faal. Kwa ajili hiyo alimsikia bwana mmoja akizungumza neno zuri akapendekezwa ambapo akasema:

“Tumechukua al-Faal kutoka mdomoni mwako.”

Abu Daawuud na Ahmad. Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “as-Swahiyhah” (02/363) kutoka kwa Abush-Shaykh katika “‘Akhlaaq-un-Nabiyy (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)”, uk. 270.

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 03/05/2020