93. Ni urefu gani kaburi linatakiwa kunyanyuliwa kutokea chini?

Swali 93: Ni urefu gani kaburi linatakiwa kunyanyuliwa kutokea chini[1]?

Jibu: Kilichowekwa katika Shari´ah ni shibiri na mfano wake. Kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) halikunyanyuliwa isipokuwa kiasi cha shibiri. Kuhusu kunyanyua sana haiuzu kutokana na yale yaliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati alipomwambia ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh):

“Usiache picha yoyote isipokuwa uiharibu wala kaburi lililonyanyuliwa isipokuwa ulisawazishe.”[2]

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/209).

[2] Muslim (969) na an-Nasaa´iy (2031).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 65
  • Imechapishwa: 06/01/2022