93. Haijuzu kuyatanguliza maneno ya yeyote kabla ya Qur-aan na Sunnah

Imaam ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Waislamu wameafikiana juu ya kwamba yule ambaye atabainikiwa na Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi haitofaa kwake kuiacha kwa sababu ya maneno ya yeyote.”[1]

´Abdullaah bin ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema kuwaambia Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum):

“Mnakaribia kuteremkiwa na mawe kutoka mbinguni. Nawaambie yale yaliyosemwa na Mtume wa Allaah na nyinyi mnanambia yale yaliyosemwa na Abu Bakr na ´Umar?”[2]

Mkiyatanguliza maneno ya Abu Bakr na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhum) kabla ya maneno ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi kunachelea juu yenu kuteremkiwa na mawe kutoka juu mbinguni. Tusemeje kwa yule mwenye kutanguliza madhehebu ya mtu fulani mbele ya Qur-aan na Sunnah? Mambo hayo yakienda kinyume na madhehebu yake au madhehebu ya mwalimu wake basi anakuwa na msimamo wa ukaidi na wala anakuwa si mwenye kuitaka. Tunamuomba Allaah afya. Mtu kama huyu kuna khatari akawa miongoni mwa wale ambao Allaah amesema juu yao:

وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ تَعْرِفُ فِي وُجُوهِ الَّذِينَ كَفَرُوا الْمُنكَرَ

“Wanaposomewa Aayah Zetu za wazi kabisa, basi utatambua katika nyuso za wale waliokufuru karaha.” (al-Hajj 22:72)

Kwa nini? Kwa sababu wanazichukia Aayah za Allaah (´Azza wa Jall). Khatari ni kubwa katika mlango huu.

Kuna khatari kubwa juu ya kichenguzi hichi na kimefichikana ndani ya nyoyo na nafsi. Kwa hivyo ni wajibu kwa muislamu aichunguze nafsi yake na kichenguzi hichi ili asiwe na kitu katika hayo au akachukia kitu katika mambo yaliyokuja kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ima akafanya hivo kwa sababu ya matamanio yaliyomo nafsini mwake, yameenda kinyume na madhehebu yake, yameenda kinyume na kipote chake au mwalimu wake. Mtu kama huyu yuko katika khatari kubwa.

[1] ”I´ilaam-il-Muwaqqi´iyn” (02/282) ya Ibn-ul-Qayyim.

[2] Ahmad (3121) na wengineo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 120-121
  • Imechapishwa: 06/12/2018