92. Bora ni kaburi linyanyuke juu ya ardhi kwa kiasi cha shibiri

Swali 92: Tunawaona watu wengi baada ya kumzika maiti wanalinyanyua kaburi lake zaidi ya shibiri. Ninapowakataza wanasema kuwa wanafanya hivo kwa ajili ya kumlinda kutokamana na mafuriko. Vivyo hivyo nawaona kuwa wanazidisha changarawe juu ya kaburi baada ya kumzika zaidi ya ule udongo wake uliotoka ndani. Vivyo hivyo wananyunyizia juu yake maji. Ni ipi hukumu ya matendo yao[1]?

Jibu: Yote haya hayana neno. Bora ni shibiri moja na mfano wake. Wakizidisha kidogo kwa changarawe au mfano wake jambo ni lenye wasaa. Ili makaburi yatambulike na yasitweze. Wakimfukia kwa udongo wake na wakaweka juu yake changarawe na wakanyanyuzia maji ili udongo ukae imara, yote haya hayana neno. Kwa sababu kufanya hivo kunalinda udongo wake na kufanya ubaki.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/208-209).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 64-65
  • Imechapishwa: 06/01/2022