92. al-Qummiy upotoshaji wake wa tisa wa an-Nisaa´

al-Qummiy amesema pindi alipokuwa akifasiri Aayah:

وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا

“Atakayemtii Allaah na  Mtume basi hao watakuwa pamoja na wale Allaah aliowaneemesha – miongoni mwa Manabii na wakweli na mashahiidi na waja wema – na uzuri ulioje kuwa pamoja na hao!”[1]

“Manabii ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wakweli ni ´Aliy, mashahidi ni al-Hasan na al-Husayn, waja wema ni maimamu na ni uzuri ulioje kuwa pamoja na hao ni al-Qaa´im[2] kutoka katika familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[3]

Wako wapi Manabii na Mitume wengine (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam)? Wako wapi mashahidi katika Maswahabah wa Muhammad na wafuasi wengine wote wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam)? Wako wapi waja wema wa Ummah huu na nyumati zengine?

Je, watu hawa watakuwa pamoja na al-Qaa´im ambaye hajawahi kupatikana na kamwe hatopatikana? Ni kina nani wataokuwa pamoja na Mitume, wakweli, mashahidi na waja wema? Raafidhwah!?!? Hakuna mwengine yeyote na khaswa khaswa Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah awaue waongo wanoakichezea shere Kitabu cha Allaah!

[1] 04:69

[2] al-Mahdiy.

[3] Tafsiyr al-Qummiy (1/142-143).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intisaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 137-138
  • Imechapishwa: 23/11/2017