90. Baada ya kumzika maiti anaombewa du´aa ya uthabiti na msamaha

Swali 90: Kumwombea du´aa ya uthabiti maiti kunakuwa kabla au baada ya kuzika[1]?

Jibu: Kunakuwa baada ya kumaliza kuzika. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapomaliza kumzika maiti basi husimama karibu naye na kusema:

“Mwombeeni msamaha ndugu yenu na mtakieni uimara; kwani hakika hivi sasa anahojiwa.”[2]

Kuhusu wakati wa kuzika mtu atasema:

بسم الله وعلى ملة رسول الله

“Kwa jina la Allaah na juu ya mila ya Mtume wa Allaah.”

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/206).

[2] Abu Daawuud (3221).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 63-64
  • Imechapishwa: 05/01/2022