90. al-Qummiy upotoshaji wake wa saba wa an-Nisaa´

al-Qummiy amesema:

“Maneno Yake:

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ رَأَيْتَ الْمُنَافِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودًا

“Wanapoambiwa: “Njooni katika yale aliyoyateremsha Allaah na kwa Mtume”, basi utawaona wanafiki wanakugeukilia mbali kwelikweli.”[1]

inawahusu maadui wa familia ya Muhammad. Aayah hii inawagusa.”[2]

Aayah hii ni kama ile iliyotangulia inawahusu wanafiki na inawagusa vilevile wale wenye kufanana na wao kama Raafidhwah Baatwiniyyah. Wao ni maadui wa Allaah, Mtume Wake na waumini wakiwemo Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na familia yake.

[1] 04:61

[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/142).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intisaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 134
  • Imechapishwa: 23/11/2017