9. Waumini wako daraja ngapi na ni zipi?

Swali 9: Waumini wamegawanyika daraja ngapi na ni zipi?

Jibu: Waumini wamegawanyika daraja tatu:

1- Aliyetangulia katika mambo ya kheri. Ni wale wenye kufanya yale ya wajibu na yaliyopendekezwa na wakajiepusha na yale ya haramu na yenye kuchukiza.

2- Wa kati na kati. Ni wale wenye kufanya yale ya wajibu na kujiepusha na yaliyoharamishwa.

3- Aliyejidhulumu nafsi. Ni wale wenye kuchanganya matendo mazuri na mabaya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamm-ul-Muhimmaat, uk. 46
  • Imechapishwa: 25/03/2017