9. Ni wajibu kwa mwanamke ajifunike mbele ya wanaume ajinabi


4- Kauli ya Allaah (Ta´ala):

لَّا جُنَاحَ عَلَيْهِنَّ فِي آبَائِهِنَّ وَلَا أَبْنَائِهِنَّ وَلَا إِخْوَانِهِنَّ وَلَا أَبْنَاءِ إِخْوَانِهِنَّ وَلَا أَبْنَاءِ أَخَوَاتِهِنَّ وَلَا نِسَائِهِنَّ وَلَا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ ۗوَاتَّقِينَ اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدًا

“Si jambo lenye kulaumika juu yao [endapo watazungumza wazi wazi na] baba zao na watoto wao wa kiume na kaka zao na watoto wa kiume wa kaka zao na watoto wa kiume wa dada zao na wanawake wenzao [wa Kiislamu] na iliyowamiliki mikono yao ya kulia. Na mcheni Allaah [enyi wanawake wote]! Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Mwenye kushuhudia.”[1]

Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) amesema:

“Wakati Allaah alipoamrisha wanawake kujifunika mbele ya wanaume ajinabi akabainisha kuwa sio wajibu kufanya hivo na wale ndugu ambao amewavua katika Suurat-un-Nuur pindi aliposema:

وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ

“Na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, baba zao, baba za waume wao…”[2]

Aayah hizi tukufu nne zinawajibisha kwa mwanamke kujifunika mbele ya wanaume ajinabi na ile Aayah ya kwanza ina nukta tano.

[1] 33:55

[2] 24:31

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hijaab, uk. 12-13
  • Imechapishwa: 26/03/2017