9. Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa Rifaa´ah al-Juhaniy

68 – ´Abdullaah bin Muhammad bin Ziyaad al-Faqiyh ametuhadithia: Muhammad bin Yahyaa ametuhadithia: Wahb bin Jariyr ametuhadithia: Hishaam ad-Dastawaa’iy ametuhadithia, kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr, kutoka kwa Hilaal bin Abiy Maymuunah, kutoka kwa ´Atwaa’ bin Yasaar aliyesema kwamba Rifaa´ah al-Juhaniy amemweleza:

“Siku moja tulikuwa nje pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mpaka tulipofika Kadiyd (au Qadiyd) watu wakaanza kumuomba idhini Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kurejea kwa familia zao. Akawapa idhini, akamuhimidi Allaah na akasema yaliyo mazuri. Kisha akasema: “Inakuweje upande wa mti ambao uko karibu zaidi na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni wenye kuchukizwa zaidi kwenu kuliko upande mwingine?” Ndipo watu wakaanza kulia. Bwana mmoja akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Atakayekuomba idhini baada ya haya ni mtenda dhambi.” Akamuhimidi Allaah na akasema yaliyo mazuri kwa mara nyingine. Kisha akasema: “Hakuna mja anayekufa ambaye anashuhudia ya kwamba hapana mungu wa kweli isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Mtume wa Allaah hali ya kuwa ni mkweli kutoka moyoni mwake kisha akatenda kati na kati isipokuwa ataingia Peponi. Ameniahidi watu elfu sabini kutoka katika Ummah wangu kuingia Peponi bila kufanyiwa hesabu wala kuadhibiwa.  Mimi nataraji hatoingia yeyote mpaka nyinyi na waliotengenea katika wake zenu na dhuriya yenu mjitengenezee makazi Peponi.” Akasema: “Kunapopita nusu ya usiku, au theluthi yake, basi hushuka Allaah (´Azza wa Jall) katika mbingu ya chini na anasema mpaka kunaingia alfajiri: “Simuulizi yeyote juu ya waja Wangu zaidi yangu Mwenyewe. Ni nani mwenye kuniomba nimuitikie? Ni nani mwenye kuniomba msamaha nimsamehe? Ni nani mwenye kuniomba nimpe?[1]

Pia al-Awzaa´iy ameipokea kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr.

[1] Ahmad (4/16).

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 146-146
  • Imechapishwa: 29/04/2020