9. Fikra za ki-Ikhwaaniy na viatu nje ya nyumba, asanteni!


Dr. ´Abdul-´Aziyz Kaamil[1] amesema:

“Walijadili na Mahmuud Shaakir kuhusu al-Ikhwaan. Akaona kuwa wengi wako juu juu ambao wamejitokeza hivi karibuni tu, washabiki ambao hawaangalii dalili na ambao wanataka kufikia natija bila ya kuthibitisha. Hali ya hewa ikazidi kutia wasiwasi zaidi na akaanza kuchukizwa na baadhi ya mienendo yao na mienendo ya al-Ikhwaan ya hapo kabla. Majadiliano yakazidi kuwa makali na hali ya joto ikapanda juu zaidi.

Upande mmoja akaona jinsi hawawaheshimu viongozi wao na juhudi zao na akaona kuwa mfumo wao una makosa. Upande mwingine akaona jinsi wako na ushabiki na ufinyu na jinsi walivo na haraka ya kuwahukumu watu hata kama itahusiana na Takfiyr na kuhalalisha kumwaga damu. Siku moja akakasirika sana na wao wakawa sugu. Akapasuka kwa khasira:

“Yule anayetaka kujifunza kwangu na kujadiliana na mimi aache kile kilichomo kichwani mwake na kuvua viatu vyake nje ya nyumba yangu.”[2]

Mara nyingi alikuwa akisema:

“Toeni vichwani mwenu fikra za Hasan al-Bannaa mlizopata kutoka kwake na vueni viatu vyenu nje ya mlango wa chumba.”

[1] Alikuwa ni kiongozi wa al-Ikhwaan.

[2] ´Aliy ´Ashmaawiy amesema:

“Mahmuud Shaakir alikuwa akiwaambia: “Kabla hamjaingia ndani ya chumba hichi toeni kilichomo kichwani mwenu na vueni viatu vyenu nje ya mlango.” (at-Taariykh as-Sirriy li Jamaa´at-il-Ikhwaan al-Muslimiyn,uk. 244)

Mwandishi: Dr. ´Abdul-´Aziyz Kaamil
Marejeo: Gazeti al-Mudhakkiraat, uk. 66-67
Mkusanyaji: Muhammad bin ´Iwadhw bin ´Abdil-Ghaniy
Chanzo: Lamahaat ´an Da´wat-il-Ikhwaan al-Muslimiyn, uk. 30-31