9. al-Halabiy anatuhumu kuwa mfumo wa Salaf umepetuka mipaka

al-Halabiy anaendeleza vita vyake vikali kwa Salafiyyuun na khaswa Rabiy´. Yeye na wenzake walikagua vitabu vyangu vinavolingania katika mfumo, ´Aqiydah na misingi ya Salaf. Malengo yao ni kuchafua mfumo mkubwa unaopatikana katika vitabu hivyo na kuwakimbiza watu navyo na wafuasi wake. Hilo limetolewa ushahidi na uhakika wa mambo, misingi, mfumo na ukaribu kwa watu wapotevu na misingi yao. Miongoni mwa ukaguzi huo ni pamoja na makala iliyoenezwa ikiitwa ”Tanaaqudhw-ush-Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy fiy Ta’swiyl Mawqifih min al-Mukhaalif wa Kashf bu´dih ´an Rusuwkh-il-Mu’asswiliyn”. Mara ya kwanza ilienezwa kwa jina lake, kisha, kwa sababu ya propaganda chafu, kwa jina la admin wa tovuti Kull-us-Salafiyyiyn. Kwa vile yeye ndiye anahusika na makala na usambazwaji wake, mjadala wangu ninauelekeza kwake na wakati mwingine vilevile kwa pote lake:

al-Halabiy amesema:

“Kwanza ni kuwa kujigonga kwa Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy haukukomeka na upande wa kielimu ilio safi. Bali umepanuka na unahusiana vilevile na msimamo wake katika pande nyinginezo. Hili linaweza kuonekana katika uhusiano wake na mafungamano yake binafsi na mimi. Mfano wa hilo ni pale ambapo Shaykh ´Aliy al-Halabiy alipoandika kitabu “Manhaj-us-Salaf as-Swaalih” basi Shaykh Rabiy´akakirudisha na kukikemea na akafanya wapumbavu na watoto kukishambulia. Kwa sababu anajua kuwa kitabu hiki kinaraddi misingi ilopetuka mipaka alio nayo Shaykh al-Madkhaliy hata kama itakuwa kwa maneno yake mwenyewe al-Madkhaliy!”[1]

1- Mimi sina misingi mingine niliyoshikamana nayo zaidi ya misingi ya Salaf. Sijaiacha na himdi zote ni za Allaah.

2- Maneno yako yanatuhumu mfumo wa Salaf kuwa na misingi yenye kupetuka mipaka. Ni jambo lisilokuwa na shaka yoyote juu ya kwamba al-Halabiy na pote lake ni miongoni mwa wenye kwenda kinyume vibaya sana na kuiraddi misingi ya Salaf.

3- Sikufanya wapumbavu wakakushambulia. Aliyekuraddi ni mtu ambaye ni mwanachuoni na ambaye ni mjuzi wa misingi ya Salaf na mambo yenye kuivunja na ni mwanachuoni katika Hadiyth na misingi yake na ana shahada ya juu ambayo si wewe wala pote lako hamna. Miongoni mwa mfumo wenu batili ni pamoja na kuonelea kuwa kila mwenye kuraddi upotofu wenu kwa hoja na dalili ni mjinga na mpumbavu.

[1] Uk. 01

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
  • Imechapishwa: 08/01/2017