Swali 89: Imepokelewa katika Hadiyth juu ya maamrisho ya kumwombea du´aa maiti baada ya kuzikwa kwake. Je, amri hii ni kwa njia ya ulazima au imependekezwa tu? Tumeona kuwa watu wameacha Sunnah hii au wajibu huu baada ya kumzika maiti[1]?
Jibu: Kumwombea du´aa ya uthabiti na msamaha maiti baada ya kuzikwa ni jambo limependekezwa na sio lazima. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapomaliza kumzika maiti basi husimama karibu naye na kusema:
“Mwombeeni msamaha ndugu yenu na mtakieni uimara; kwani hakika hivi sasa anahojiwa.”[2]
[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/205).
[2] Abu Daawuud (3221).
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 63
- Imechapishwa: 04/01/2022