88. Ni ipi hukumu ya kuweka kuti la mtende la kijani juu ya kaburi la maiti?


Swali 88: Ni ipi hukumu ya kuweka kuti la mtende la kijani juu ya kaburi la maiti?

Jibu: Haikuwekwa katika Shari´ah kufanya hivo. Bali ni Bid´ah. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliweka kuti juu ya makaburi mawili baada ya kuwa Allaah (Subhaanah) amekwishamfunulia kwamba wanaadhibiwa watu wa makaburi hayo mawili na hakuyaweka juu ya makaburi mengine. Hivyo ikapata kujulikana kutofaa kuyaweka juu ya makaburi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu basi atarudishiwa mwenyewe.”[1]

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tena:

“Yeyote atakayezua katika amri yetu hii yale yasiyokuwemo basi atarudishiwa mwenyewe.”[2]

Kuna maafikiano juu ya usahihi wake.

Vivyo hivyo haifai kuandika juu ya kaburi wala kuweka maua juu yake kutokana na Hadiyth mbili zilizotajwa. Jengine ni kwamba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikataza kuyaweka chokaa makaburi, kujenga juu yake, kuketi juu yake na kuandika juu yake.

[1] Muslim (1718).

[2] al-Bukhaariy (2697) na Muslim (1718).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 62
  • Imechapishwa: 04/01/2022