88. Inatosha ukafiri wa anayechukia kitu kimoja tu katika Shari´ah

Kwa kifupi ni kwamba yule ambaye ndani ya moyo wake kuna chuki kwa kitu chochote katika mambo yaliyotoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), hakika hii ni dalili ya unafiki wake na kutokuwa na imani. Haijalishi kitu japokuwa atadai kuwa na imani na kuzitendea kazi Hadiyth hizi kwa uinje, maadamu anzichukia ndani ya moyo wake, basi hakika hiki ni kichenguzi miongoni mwa vichenguzi vya Uislamu. Aayah hii ndio dalili juu ya hilo.

الَّذِينَ كَفَرُوا فَتَعْسًا لَّهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ

“Wale waliokufuru, basi ni maangamizo kwao na atayapoteza matendo yao. Hivyo kwa sababu wao wameyachukia ambayo ameteremsha Allaah, hivyo ameyabatilisha matendo yao.”[1]

Mwishoni mwa Suurah imekuja:

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ اتَّبَعُوا مَا أَسْخَطَ اللَّـهَ وَكَرِهُوا رِضْوَانَهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ

”Hivyo kwa kuwa wao wamefuata yale yanayomghadhibisha Allaah na wakachukia radhi Zake. Hivyo akayaporomosha matendo yao.” (Muhammad 47:28)

Hii ndio sababu. Hiki ni kichenguzi miongoni mwa vichenguzi vya Uislamu pindi mtu atachukia kitu katika mambo yaliyokuja kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

… kuchukia kitu… –  Bi maana sio lazima achukie yote yaliyokuja kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Inatosha kuchukia baadhi ya mambo. Iwapo kwa mfano atachukia baadhi ya Hadiyth Swahiyh zilizothibiti, matendo yake yote yanaharibika na Uislamu wake unachenguka. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hatoamini mmoja wenu mpaka matamanio yake yawe ni yenye kufuata yale niliyokuja nayo.”[2]

Matamanio yao hayakuwa ni yenye kufuata na kujisalimisha yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa ajili hiyo ndio maana Allaah akayaharibu matendo yao. Aayah hii inaitolea ushahidi Hadiyth hapo huu.

[1] 47:08-09

[2] Tazama “Jaamiy´-ul-´Uluum wal-Hikam” ya Ibn Rajab (2/393).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 116
  • Imechapishwa: 27/11/2018