88. al-Qummiy upotoshaji wake wa tano wa an-Nisaa´


al-Qummiy amesema pindi alipokuwa akifasiri Aayah:

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُؤْمِنُونَ بِالْجِبْتِ وَالطَّاغُوتِ وَيَقُولُونَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا هَـٰؤُلَاءِ أَهْدَىٰ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا سَبِيلًا

“Je, huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanaamini masanamu na ukafiri na wanasema juu ya wale waliokufuru: wameongoka zaidi katika njia kuliko wale walioamini.”[1]

“Imeteremshwa wakati washirikina walipowauliza mayahudi: “Je, dini yetu ni bora kuliko ya Muhammad?” Mayahudi wakajibu: “Dini yenu ndio bora.” Imepokelewa vilevile kwamba imeteremshwa kuhusu wale ambao waliwapokonya familia ya Muhammad haki yao na wakawahusudu nafasi zao. Allaah amesema juu yao:

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ ۖ وَمَن يَلْعَنِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ نَصِيرًا أَمْ لَهُمْ نَصِيبٌ مِّنَ الْمُلْكِ فَإِذًا لَّا يُؤْتُونَ النَّاسَ نَقِيرًا

“Hao ndio wale waliolaaniwa na Allaah na yule ambaye Allaah kamlaani basi hatopata wa kumnusuru. Au wanayo sehemu ya ufalme? [Mambo yangekuwa hivo], basi wasingeliwapa watu kiasi cha kitone cha kokwa ya tende.”[2]

Kisha Akasema:

أَمْ يَحْسُدُونَ النَّاسَ عَلَىٰ مَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ ۖ فَقَدْ آتَيْنَا آلَ إِبْرَاهِيمَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَآتَيْنَاهُم مُّلْكًا عَظِيمًا

“Au wanawahusudu watu kwa yale aliyowapa Allaah katika fadhila Zake? Bila shaka Tuliwapa kizazi cha Ibraahiym Kitabu na hekima na tukawapa ufalme mkubwa.”[3]

Bi maana wanamuhusudu kiongozi wa waumini na maimamu kwa ajili ya ukhaliyfah waliopewa baada ya utume?”[4]

Aayah inabainisha ukafiri, ukaidi na uadui wa mayahudi kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wale wenye kuamuamini pamoja na hasadi yao kwake, kwa Maswahabah wake na Ummah wake. al-Qummiy ameashiria hilo, lakini madhehebu yake ya ki-Baatwiniy na ya ki-Raafidhwiy hayakumuwezesha jengine isipokuwa kuzielekeza Aayah kwa Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kuwasema na kuwazulia uongo na huku kujifanya kutumia familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na haki zao wanazodaiwa zilizopokonywa. Anazipindisha laana zilizoelekezwa kwa mayahudi kwenda kwa Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilihali uhalisia ni kwamba yeye na watu mfano wake ndio wanaostahiki kulaaniwa, kukoseshwa nusura na kudhalilishwa duniani na Aakhirah.

[1] 04:51

[2] 4:52-53

[3] 4:54

[4] Tafsiyr al-Qummiy (1/140).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intisaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 131
  • Imechapishwa: 20/11/2017