87. Ni ipi hukumu ya kuweka alama juu ya kaburi?


Swali 87: Ni ipi hukumu ya kuweka alama juu ya kaburi[1]?

Jibu: Hakuna neno kuweka alama, kama vile jiwe au mfupa, juu ya kaburi ili litambulike pasi na kuandika wala kuweka namba. Kwa sababu kuweka namba ni kuandika. Kumesihi makatazo kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kuandika juu ya kaburi. Kuhusu kuweka jiwe juu ya kaburi, kupaka rangi nyeusi au ya najo juu ya jiwe ili iwe alama ya mwenye nalo haina neno. Kwa sababu imepokelewa ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alilitambua kaburi la ´Uthmaan bin Madh´uun kwa alama.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/200).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 61
  • Imechapishwa: 03/01/2022