87. Ndio maana mafusaki wanayapenda madhehebu ya Murji-ah

Imaam Ibn Abiy Daawuud (Rahimahu Allaah) amesema:

ولا تكُ مُرْجيًّا لَعُوبا بدين

35 – Usiwe Murjiy´ anayecheza na dini yake

ألاَ إِنمَا المُرْجِي بِالدينِ يَمْزحُ

     Eleweni hakika Murjiy´ kweli anaifanyia mzaha dini

وقلْ إنمَا الإِيمانُ قولٌ ونِيةٌ

36 – Sema kuwa imani ni maneno na nia

وفعلٌ عَلَى قولِ النبِي مُصَرحُ

     na kitendo kutokana na [ushahidi wa] maneno ya Mtume yaliyo wazi

ويَنْقُصُ طوراً بالمَعَاصِي وتَارةً

37 – Inapungua kwa maasi wakati fulani, na wakati mwingine

بِطَاعَتِهِ يَنمِي وفي الوَزْنِ يَرْجَحُ

     inaongezeka kwa utiifu na inakuwa na uzito kwenye mizani

MAELEZO

Murji-ah ndio kundi la upande wa pili linalokabiliana na Khawaarij. Wameitwa ´Murji-ah` kutokamana na neno “Irjaa´” ambayo maana yake ni kuchelewesha. Kwa kuwa wao wamechelewesha matendo katika imani na wakasema kuwa matendo hayaingii katika imani. Wao wanaonelea kuwa iwapo mtu ataamini kwa moyo wake lakini asifanye kitu; asiswali, asitoe zakaah, asifanye maamrisho na kujiepusha na mambo ya haramu ni muumini mwenye imani kamilifu. Hii ni ´Aqiydah batili inayokana matendo kabisa.

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“Usiwe Murjiy´ anayecheza na dini yake.”

Kwa sababu ´Aqiydah ya Murji-ah ni kucheza na dini. Wanaona kuwa mja anakuwa muumini ingawa hakufanya kitu; hata kama ataacha swalah, ataacha kufunga, ataacha kutoa zakaah, kuhiji hata kama hatofanya kitu chochote katika maisha yake yote. Sivyo tu bali hata kama atafanya ya haramu yote. Hii ni ´Aqiydah batili. Kwa ajili hii watenda madhambi na maasi wanafurahi kwa ´Aqiydah hii na kuisapoti. Kwa sababu yanaendana nao kwa njia ya kwamba wanapata kufanya wanachokitaka na wakati huohuo bado wako na imani zao kwa mujibu wa Murji-ah. Wanaofuata hawaa, matamanio na maasi wanafurahi kwa ´Aqiydah hii. ni ´Aqiydah iliyojengwa juu ya kucheza na dini.

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“Eleweni hakika Murjiy´ kweli anaifanyia mzaha dini.”

Bi maana Murji-ah wanacheza na dini na wanayaharibu maamrisho na makatazo. Kwa mujibu wa ´Aqiydah yao hakuna haja ya maamrisho na makatazo. Huku ni kucheza na dini ya Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 185-186
  • Imechapishwa: 13/01/2024