Kinachoshangaza ni kwamba watu hawa wamezijenga ´Aqiydah zao juu ya falsafa na kanuni za kimantiki na wanasema kuwa haya ndio yanafidisha yakini. Sambamba na hilo wanaona kuwa maneno ya Allaah hayafidishi yakini na Sunnah haifidishi yakini kwa mtazamo wao. Huu ni upotofu na maangamivu.

Ama Ahl-ul-Haqq na Ahl-us-Sunnah wanasema kwamba yale yote yaliyothibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yanafidisha yakini na elimu na yanatumiwa kama hoja na dalili katika mambo ya ´Aqiydah, ´ibaadah na mu´amala. Hakuna tofauti katika hayo. Hii ndio njia ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 115-116
  • Imechapishwa: 27/11/2018