86. Sunnah ni kutoa Tasliym nyepesi katika swalah ya jeneza


85- Sunnah atoe Tasliym katika jeneza kimyakimya nyepesi. Ni mamoja imamu na wale waliokowa nyuma yake. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya Abu Umaamah katika masuala haya kwa tamko:

“Kisha atoe Tasliym kimyakimya nyepesi pale anapomaliza. Sunnah afanye aliyeko nyuma ya imamu mfano wa vile alivofanya imamu wake.”

Inayo shahidi ambayo imenasibishwa kwa Swahabah. Ameipokea al-Bayhaqiy (04/43) kutoka kwa Ibn ´Abbaas kwamba amesema:

“Alikuwa akitoa Tasliym yenye sauti ndogo.”

Cheni ya wapokezi wake ni nzuri.

Kisha ikapokelewa kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Umar kwamba amesema.

“Alikuwa anapoliswali janeza basi huleta Tasliym mpaka awasikilizishe walio nyuma yake.”

Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh[1].

[1] Kana kwamba kutofautiana kwa Aathaar hizi mbili ndio maana zikatofautiana kauli za Hanaabilah juu ya masuala haya. Imetajwa katika “al-Inswaaf” (05/523):

“Imesemwa katika “al-Furuu´”: Dhahiri ya maneno ya maswahiba [Hanaabilah] ni kwamba imamu atoe Tasliym kwa sauti. Na dhahiri ya maneno ya Ibn-ul-Jawziy ni kwamba imamu asome kimyakimya. Kisha ikanukuliwa kutoka kwa “al-Madhhab” na “Masbuuk-udh-Dhahab” yanayolenganisha juu ya maneno ya Ibn-ul-Jawziy, na ndilo lenye nguvu zaidi kutokana na Hadiyth ya Abu Umaamah.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 164-165
  • Imechapishwa: 08/02/2022