85. Kuhamisha alama ya kaburi la kale kwenda kaburi la sasa

Swali 85: Je, inafaa kuhamisha alama ya kaburi la zamani na kuipeleka katika kaburi jipya[1]?

Jibu: Kinachonidhihirikia mimi kutoka katika Shari´ah ya zamani ni kwamba hilo halifai. Ni alama ya kaburi la kwanza. Wakiiona watu wanaliheshimu na hivyo hawalikanyagi, hawaketi juu yake na wala hawawezi juu yake uchafu. Kwa hiyo kuihamisha ni kupoteza ile heshima yake na kaburi jipya halina ulazima wa alama hiyo. Bali linaweza kuwekewa alama nyingine. Kusipopatikana kitu basi hapana neno likabaki pasi na alama muda wa kuwa limenyanyuliwa juu ya kaburi kwa kiasi cha shibiri kwa mujibu wa sifa ya kaburi.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/198-199).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 60
  • Imechapishwa: 01/01/2022