84- Inafaa kutosheka na Tasliym ya kwanza peke yake. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza:

“Hakika Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimswalia maiti ambapo akampigia Takbiyr nne na akatoa Tasliym moja.”

Ameipokea ad-Daaraqutwniy (191), al-Haakim (01/360) na al-Bayhaqiy kutoka kwake (04/43) kupitia kwa Abul-´Anbas kutoka kwa baba yake kutoka kwake.

Cheni ya wapokezi wake ni nzuri, kama nilivyobainisha katika “at-Ta´liyqaat al-Jiyaad.”

Vilevile inatolewa ushahidi na Mursal ya ´Atwaa´ bin as-Saa-ib ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alilitolea jeneza moja Tasliym moja.

Ameipokea al-Bayhaqiy ikiwa na cheni ya wapokezi pungufu. Lakini linatiliwa nguvu na kitendo cha jopo la Maswahabah waliokuwa wakiyafanya haya. al-Haakim amesema punde tu baada yake:

“Yamesihi mapokezi katika jambo hili kutoka kwa ´Aliy bin Abiy Twaalib, ´Abdullaah bin ´Umar, ´Abdullaah bin ´Abbaas, Jaabir bin ´Abdillaah, ´Abdullaah bin Abiy Awfaa na Abu Hurayrah kwamba walikuwa wakitoa juu ya jeneza Tasliym moja.”

adh-Dhahabiy ameafikiana naye na al-Bayhaqiy amezitaja kwa cheni ya wapokezi nyingi katika Aathaar hizi na akaongeza juu yao:

“Waathilah bin al-Asqaa´, Abu Umaamah na wengineo.”

Kusema kuwa upokezi wa Ibn Abiy Awfaa ni Swahiyh kwa njia ya kuachia ni jambo lina walakini. Kwani katika cheni ya wapokezi wake yumo al-Jarraah bin Maliyh, ambaye ni mnyonge kama ilivyotangulia punde kidogo. Isipokuwa ikiwa kama al-Haakim ameipata njia nyingine kutoka katika njia nyingine, jambo ambalo silifikirii.

Kutokana na Aathaar hizi Imaam Ahmad ameonelea katika yale yaliyotangaa zaidi kwake. Abu Daawuud amesema katika “al-Masaa-il” yake (153):

“Nilimsikia Ahmad akiulizwa kuhusu Tasliym juu ya jeneza. Akajibu: “Namna hii.” Akaipinda shingo yake upande wa kulia [na akasema:

السلام عليكم ورحمة الله

“Amani na baraka za Allaah ziwe juu yenu.]”

Nyongeza:

وبركاته

“… na baraka Zake.”

katika Tasliym hii ni jambo limewekwa katika Shari´ah tofauti na baadhi yao. Kwa sababu limethibiti katika baadhi ya njia za Hadiyth ya Ibn Mas´uud iliyokwishatangulia kuhusu Tasliym mbili katika swalah ya faradhi. Mfano wake katika masuala haya ni swalah ya jeneza, kama ilivyotangulia. Ibn Qaasim-il-Ghazziy ametaja katika maelezo yake kwamba imependekezwa kuiweka hapa katika Tasliym mbili. al-Baajuuriy akamraddi katika “al-Haashiyah” yake (01/431) na akaonelea kuwa haikusuniwa mahala hapa wala katika swalah ya faradhi. Usawa ni yale tuliyoyataja.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 163-164
  • Imechapishwa: 08/02/2022