85. al-Qummiy upotoshaji wa pili wa an-Nisaa´


al-Qummiy amesema pindi alipokuwa anafasiri Aayah:

يَوْمَئِذٍ يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَعَصَوُا الرَّسُولَ لَوْ تُسَوَّىٰ بِهِمُ الْأَرْضُ وَلَا يَكْتُمُونَ اللَّـهَ حَدِيثًا

“Siku hiyo wale waliokufuru na wakamuasi Mtume watatamani lau ardhi isawazishwe juu yao;  na wala hawatoweza kumficha Allaah chochote katika yale waliyosema [au kufanya].”[1]

“Watatamani wale  waliompokonya uongozi kiongozi wa waumini lau ardhi isawazishwe juu yao siku ambayo walikusanyika kumpora na wala hawakuficha chochote katika yale yaliyosemwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu yake.”[2]

Tazama upotoshaji huu wa ki-Baatwiniy. Aayah inawazungumzia wale makafiri waliomkadhibisha Allaah na Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ile khofu watayokuwa nayo siku ya Qiyaamah. Raafidhwiy huyu anaipachika kwa Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao wamemuamini Allaah, Mtume wake, Vitabu vyake na kadhalika na wakapambana katika njia ya Alllaah kwa mali zao na nafsi zao. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekufa akiwa radhi nao.

[1] 04:42

[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/139).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 128
  • Imechapishwa: 07/11/2017