Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Hiyo ndio ile ambayo alimshusha kutoka ndani yake Aadam Mtume na khalifa Wake kwenda ardhini, jambo ambalo lilitangulia katika ile elimu Yake ya milele.

MAELEZO

Pepo ni ile ambayo Allaah alimkaza ndani yake Aadam au ni nyingine? Wanachuoni wametofautiana. Maoni sahihi ni kwamba ni Pepo hiyohiyo. Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hiyo ndio ile ambayo alimshusha kutoka ndani yake Aadam Mtume Wake na khalifa wake kwenda ardhin… “

Kwa sababu Aadam ni Nabii aliyezungumzishwa. Lakini neno “khalifa” linahitajia kuangaliwa vizuri kwa sababu Allaah hana khalifa – bali Allaah ndiye khalifa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika du´aa yake ya safarini:

اللهم أنت الصاحب في السفر والخليفة في الأهل

“Ee Allaah! Hakika Wewe ndiye unayesuhubiana nami katika safari na mchungaji wa familia yangu.“[1]

Hakuna yeyote anayechukua nafasi ya Allaah ambaye ni naibu Wake; watu ndio huwa naibu wao kwa wao. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَهُوَ الَّذِي جَعَلَكُمْ خَلَائِفَ الْأَرْضِ

“Naye ndiye aliyekufanyeni makhalifa wa ulimwenguni.”[2]

Bi maana baadhi baadaye mnachukua nafasi za wengine. Kuhusu maneno Yake (Ta´ala):

إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً

“Hakika Mimi nitaweka katika ardhi khalifa.”[3]

yanalenga wale viumbe wengine waliokuwa wakiishi ardhini kabla yake, haina maana kwamba wanachukua nafasi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Isipokuwa ikiwa kama mtunzi (Rahimahu Allaah) analenga maana hii, basi hapo kuna mashiko.

[1] Muslim (1342).

[2] 6:165

[3] 2:30

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 62-63
  • Imechapishwa: 19/08/2021