83. Mtume na Maswahabah walipigana na watu waliokuwa wakishuhudia ya kwamba hakuna mungu wa haki ila Allaah

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Ndio maana hawa wajinga wanatakiwa kuambiwa: “Ni jambo linalojulikana ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwapiga vita mayahudi na akawafanya mateka licha ya kuwa wao wanasema “Hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah”. Kadhalika Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walipigana vita na Banuu Haniyfah pamoja na kuwa wanasema ” Hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah”, wanaswali na kudai Uislamu. Vilevile wale aliowaunguza kwa moto ´Aliy bin Abiy Twaalib.

MAELEZO

Haya ni majibu juu ya shubuha zilizotangulia walizoleta wajinga hawa. Majibu yako ifuatavyo:

1 – Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwapiga vita mayahudi na akawafanya mateka licha ya kuwa wanasema hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah.

2 – Maswahabah waliwapiga vita Banuu Haniyfah pamoja na kwamba wanashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, wanaswali na kudai kuwa ni waislamu.

3 – Wale ambao ´Aliy bin Abiy Twaalib aliwachoma kwa moto walikuwa wakishuhudia pia kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 92
  • Imechapishwa: 28/11/2023