83. Mitume wametumwa wakiwa ni wenye kutoa bishara njema na wenye kuonya

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Allaah ametuma Mitume wote wakiwa ni wenye kutoa bishara njema na kuonya. Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

رُّسُلًا مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى اللَّـهِ حُجَّةٌ بَعْدَ الرُّسُلِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا

“Mitume ni wabashiriaji na waonyaji ili pasikuweko kutoka kwa watu hoja yoyote juu ya Allaah baada ya kutumizwa Mitume. Allaah ni Mwenye nguvu kabisa asiyeshindika, Mwenye hekima.” (an-Nisaa´ 04 : 165)

MAELEZO

Shaykh (Rahimahu Allaah) amebainisha kuwa Allaah amewatuma Mitume wote hali ya kuwa ni wenye kutoa bishara njema na wenye kuonya. Amesema (Ta´ala):

رُّسُلًا مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى اللَّـهِ حُجَّةٌ بَعْدَ الرُّسُلِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا

“Mitume ni wabashiriaji na waonyaji ili pasikuweko kutoka kwa watu hoja yoyote juu ya Allaah baada ya kutumizwa Mitume. Allaah ni Mwenye nguvu kabisa asiyeshindika, Mwenye hekima.”

Wanampa bishara njema ya Pepo kwa wale wenye kuwatii na wanawaonya wale wenye kwenda kinyume na wao kwa Moto.

Kuna hekima kubwa juu ya kuwatumiliza Mitume. Muhimu zaidi ni watu wasimamiwe na hoja ili wasipate kuwa na udhuru wowote kwa Allaah baada ya kutumilizwa Mitume.  Amesema (Ta´ala):

لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى اللَّـهِ حُجَّةٌ بَعْدَ الرُّسُلِ

“Ili pasikuweko kutoka kwa watu hoja yoyote juu ya Allaah baada ya kutumizwa Mitume.”

Hekima nyingine ni kutimia neema za Allaah kwa waja Wake. Akili ya mtu, vovyote itakavyokuwa, haiwezi katu kuzifahamu zile haki zote kwa ufafanuzi  ambazo ni maalum kwa Allaah (Ta´ala). Pia haiwezi vilevile katu kuzifahamu zile sifa kamilifu za Allaah (Ta´ala) na wala haiwezi kuyafahamu majina Yake mazuri mno. Kwa ajili hiyo Allaah akawatumiliza Mitume (´alayhim-us-Swalaatu was-Salaam) wakiwa ni wenye kutoa bishara njema na kuonya. Akawateremshia Vitabu kwa haki, ili wapate kuhukumu kati ya watu kwa yale waliyotofautiana baina yao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 148-149
  • Imechapishwa: 04/06/2020