83. Kusomea mchanga wa kaburi na kuuweka juu ya sanda ya maiti

Swali 83: Imepokelewa katika “at-Targhiyb wat-Tarhiyb”:

“Anapofariki maiti basi chota udongo kutoka katika kaburi lake na msomee baadhi ya Aayah – sizikumbuki – kisha umimine juu ya sanda yake na hivyo hatoadhibiwa ndani ya kaburi lake.”

Ni upi usahihi wa hilo[1]?

Jibu: Hiki ni kitu kisichokuwa na msingi wowote. Bali ni Bid´ah na maovu. Haijuzu kufanya hivo wala halina faida. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwawekea Ummah wake Shari´ah hiyo. Kilichosuniwa ni muislamu aoshwe pindi anapokufa, avikwe sanda, aswaliwe halafu azikwe katika makaburi ya waislamu. Pia imesuniwa kwa ambaye amehudhuria mazishini kumwombea du´aa ya msamaha na kumthibitisha juu ya haki baada ya kumaliza kumzika. Hivo ndivo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifanya na akiamrisha.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/197).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 58
  • Imechapishwa: 01/01/2022