83. al-Qummiy upotoshaji wa kwanza wa an-Nisaa´


al-Qummiy amesema kuhusiana na Aayah:

فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهِيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ شَهِيدًا

”Basi itakuwaje [siku ambayo] Tutakapoleta kutoka kila Ummah shahidi na tukakuleta wewe pia kuwa shahidi juu ya hawa.”[1]

فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهِيدٍ

”Basi itakuwaje [siku ambayo] Tutakapoleta kutoka kila Ummah shahidi… ”

Bi maana maimamu:

وَجِئْنَا بِكَ

”… na tukakuleta wewe pia… ”

Bi maana Muhammad:

عَلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ شَهِيدًا

”… kuwa shahidi juu ya hawa.”

 Bi maana kwa maimamu. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atashuhudia juu ya maimamu na maimamu watakuwa ni mashahidi juu ya watu.”[2]

Tazama namna ambavyo anakengeusha Aayah hii kwa njia ya ki-Baatwiniy na kupoteza haki ya Mtume wa Allaah (Swalla Alalahu ´alayhi wa sallam) na ngazi yake. Mtume (Swalla Alalahu ´alayhi wa sallam) ambaye ametumwa kwa watu wote hali ya kuwa ni mwenye kutoa bishara njema na mwenye kuonya atashuhudia tu juu ya watu watatu waliokuwa wakiishi katika wakati wake na watu wengine tisa baada ya kufa kwake? Je, maimamu ndio watakaobeba jukumu hili kubwa na kushuhudia juu watu wengine wote waliobaki? Wanapoteza vilevile haki na nafasi za Mitume wengine. Kwa mujibu wao Mitume hawana haki yoyote ya kushuhudia juu ya watu wao. Allaah amewapa haki hii maimamu kwa ajili ya kuwakirimu Raafidhwah.

Maana ya Aayah iko wazi kama jua. Maana yake ni kwamba Allaah atawafufua watu kwa ajili ya hesabu na malipo na atawaleta Mitume wote kila mmoja ashuhudie kwamba alifikisha ujumbe wa Allaah.

[1] 04:41

[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/139).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 125
  • Imechapishwa: 07/11/2017