Aliyoteremsha Allaah yamegawanyika aina mbili:

1- Ya kwanza: Qur-aan. Huu ndio Wahy wa kwanza na chanzo cha kwanza miongoni mwa vyanzo vya Uislamu.

2- Ya pili: Ni Sunnah aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu ni Wahy kutoka kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa). Allaah (Jalla wa ´Alaa) anasema kumwambia Mtume wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ

”Hatamki kwa matamanio yake. Hayakuwa ayasemayo isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa kwake.” (an-Najm 53:03-04)

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ

”Kile alichokupeni Mtume basi kichukueni na kile alichokukatazeni basi kiacheni. Mcheni Allaah! Hakika Allaah ni mkali wa kuadhibu.” (al-Hashr 59:07)

Sunnah ndio Wahy wa pili na ndio chanzo cha pili katika vyanzo ya Uislamu na hukumu za Kishari´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 111
  • Imechapishwa: 20/11/2018