Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Yule mwenye kukanusha kufufuliwa anakufuru. Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

زَعَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَن لَّن يُبْعَثُوا ۚ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبْعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلْتُمْ ۚ وَذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ

”Waliokufuru wamedai kwamba hawatofufuliwa kamwe. Sema: “Bali hapana! Naapa kwa Mola wangu, bila shaka mtafufuliwa, kisha mtajulishwa kwa yale yote mliyoyatenda; na hayo kwa Allaah ni mepesi.” (at-Taghaabuun 64 : 07)

MAELEZO

Yule mwenye kupinga kufufuliwa ni kafiri. Amesema (Ta´ala):

وَقَالُوا إِنْ هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا وَمَا نَحْنُ بِمَبْعُوثِينَ وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ وُقِفُوا عَلَىٰ رَبِّهِمْ ۚ قَالَ أَلَيْسَ هَـٰذَا بِالْحَقِّ ۚ قَالُوا بَلَىٰ وَرَبِّنَا ۚ قَالَ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ

“Na walisema: “Haya si chochote isipokuwa ni maisha tu ya dunia na wala sisi hatutofufuliwa.” Na lau ungeliona pale watakaposimamishwa mbele ya Mola wao atasema: “Je, haya si ya kweli?” Watasema: “Ndio, tunaapa kwa Mola wetu!” Atasema: “Basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyakanusha.” (al-An´aam 06 : 29-30)

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ الَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ وَمَا يُكَذِّبُ بِهِ إِلَّا كُلُّ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ كَلَّا ۖ بَلْ ۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ كَلَّا إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ ثُمَّ إِنَّهُمْ لَصَالُو الْجَحِيمِ ثُمَّ يُقَالُ هَـٰذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ

”Ole wao siku hiyo kwa wakadhibishaji, ambao wanaikadhibisha siku ya Malipo! Na haikadhibishi isipokuwa kila mwenye kuvuka mipaka, mtendaji dhambi, anaposomewa Aayah Zetu, husema: “Visa vya watu wa kale!” Hapana! Bali imetia kutu juu ya nyoyo zao yale waliyokuwa wakiyachuma! Hapana, hakika wao siku hiyo watazuiwa kutokamana na Mola wao. Kisha hakika wao bila shaka wataingizwa wachomeke Motoni, halafu itasemwa: “Haya ndio yale mliyokuwa mkiyakadhibisha!” (al-Mutwaffifiyn 83 : 10-17)

بَلْ كَذَّبُوا بِالسَّاعَةِ ۖ وَأَعْتَدْنَا لِمَن كَذَّبَ بِالسَّاعَةِ سَعِيرًا

“Bali wameikadhibisha Saa – na Tumeandaa kwa anayeikadhibisha Saa, Moto uwakao kwa nguvu.”  (al-Furqaan 25 : 11)

وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ وَلِقَائِهِ أُولَـٰئِكَ يَئِسُوا مِن رَّحْمَتِي وَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

“Na wale waliozikanusha Aayah za Allaah na kukutana Naye, hao wamekata tamaa na rehema Yangu na hao watapata adhabu iumizayo.” (al-´Ankabuut 29 : 23)

Shaykh ametumia dalili hili kwa maneno Yake (Ta´ala):

زَعَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَن لَّن يُبْعَثُوا ۚ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبْعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلْتُمْ ۚ وَذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ

”Waliokufuru wamedai kwamba hawatofufuliwa kamwe. Sema: “Bali hapana! Naapa kwa Mola wangu, bila shaka mtafufuliwa, kisha mtajulishwa kwa yale yote mliyoyatenda; na hayo kwa Allaah ni mepesi.”

Wakanushaji hawa wanakinaishwa kwa njia ifuatayo:

1- Kufufuliwa kumepokelewa mapokezi mengi kutoka kwa Manabii na Mitume katika vile vitabu vya kiungu na Shari´ah za kimbingu. Haya yamekubaliwa na nyumati zao. Vipi basi mnaweza kukanusha hilo wakati nyinyi mnaamini yale mnayonakiliwa kutoka kwa mwanafalsafa au mwananadharia fulani? Maneno haya hayakufikia mapokezi mengi kama jinsi yalivo ya kufufuliwa na wala hayakushuhudiliwa na uhakika wa mambo.

2- Kufufuliwa kumethibitishwa na akili kwa njia nyingi:

1- Hakuna yeyote anayekanusha kwamba alikuwa si mwenye kuumbwa kabla ya kutokuweko kwake. Kwa hivyo Yule aliyemuumba baada ya kutokuweko kwake basi ana haki zaidi ya kuweza kumrudisha. Amesema (Ta´ala):

وَهُوَ الَّذِي يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَهُوَ أَهْوَنُ عَلَيْهِ

“Naye ndiye Aliyeanzisha uumbaji kisha anaurudisha; nayo ni mepesi mno Kwake.” (ar-Ruum 30 : 27)

كَمَا بَدَأْنَا أَوَّلَ خَلْقٍ نُّعِيدُهُ ۚ وَعْدًا عَلَيْنَا ۚ إِنَّا كُنَّا فَاعِلِينَ

“Kama Tulivyoanza uumbaji umbo la mwanzo tutalirudisha – hiyo ni ahadi juu Yetu hakika Sisi tumekuwa ni Wenye kufanya!” (al-Anbiyaa´ 21 : 104)

2- Hakuna yeyote anayepinga ukubwa na uzuri wa mbingu na ardhi. Kwa hivyo kuna uwezekano mkubwa kwa Yule aliyeviumba vivyo hivyo akawaumba na kuwarudisha watu. Allaah (Ta´ala) amesema:

لَخَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ أَكْبَرُ مِنْ خَلْقِ النَّاسِ

“Bila shaka uumbaji wa mbingu na ardhi ni mkubwa zaidi kuliko uumbaji wa watu.” (Ghaafir 40 : 57)

أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَلَمْ يَعْيَ بِخَلْقِهِنَّ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ ۚبَلَىٰ إِنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

“Je, hawaoni kwamba Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi na wala hakuchoka kwa kuziumba kwake, kwamba ni muweza wa kuwafufua wafu? Bila shaka, hakika Yeye juu ya kila jambo ni muweza!” (al-Ahqaaf 46 : 33)

أَوَلَيْسَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يَخْلُقَ مِثْلَهُم ۚ بَلَىٰ وَهُوَ الْخَلَّاقُ الْعَلِيمُ إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ

“Je, Yule aliyeumba mbingu na ardhi mnaona hana uwezo wa kuumba mfano wao? Bila shaka! Naye ni Mwingi wa kuumba, Mjuzi wa yote. Hakika amri Yake anapotaka kitu chochote kile, basi hukiambia: “Kuwa!” – nacho kikawa.” (Yaa Siyn 36 : 81-82)

3- Kila ambaye ana busara anaiona namna ardhi inavokufa kame na mimea yake imekauka. Wakati mvua inaponyesha juu yake, inakuwa ni yenye rutuba na ikaihuisha baada ya kufa kwake. Yule ambaye ni Muweza wa kuihuisha ardhi baada ya kufa kwake, vivyo hivyo ni Muweza wa kuwahuisha wafu na kuwafufua. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمِنْ آيَاتِهِ أَنَّكَ تَرَى الْأَرْضَ خَاشِعَةً فَإِذَا أَنزَلْنَا عَلَيْهَا الْمَاءَ اهْتَزَّتْ وَرَبَتْ ۚ إِنَّ الَّذِي أَحْيَاهَا لَمُحْيِي الْمَوْتَىٰ ۚ إِنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

“Miongoni mwa alama Zake ni kwamba utaona ardhi imenyongeka, basi tunapoiteremshia maji, hutaharaki na kuumuka. Bila shaka Yule aliyeihuisha ni Mwenye kuhuisha wafu, hakika Yeye juu ya kila jambo ni muweza.”

3- Allaah (Ta´ala) ametueleza ya kwamba hisia na uhalisia wa mambo umeshuhudilia kufufuliwa pale ambapo wafu watakapofufuliwa. Allaah (Ta´ala) ametaja jambo hili sehemu tano katika Suurah “al-Baqarah”. Moja wapo:

أَوْ كَالَّذِي مَرَّ عَلَىٰ قَرْيَةٍ وَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا قَالَ أَنَّىٰ يُحْيِي هَـٰذِهِ اللَّـهُ بَعْدَ مَوْتِهَا ۖ فَأَمَاتَهُ اللَّـهُ مِائَةَ عَامٍ ثُمَّ بَعَثَهُ ۖ قَالَ كَمْ لَبِثْتَ ۖ قَالَ لَبِثْتُ يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ ۖ قَالَ بَل لَّبِثْتَ مِائَةَ عَامٍ فَانظُرْ إِلَىٰ طَعَامِكَ وَشَرَابِكَ لَمْ يَتَسَنَّهْ ۖ وَانظُرْ إِلَىٰ حِمَارِكَ وَلِنَجْعَلَكَ آيَةً لِّلنَّاسِ ۖ وَانظُرْ إِلَى الْعِظَامِ كَيْفَ نُنشِزُهَا ثُمَّ نَكْسُوهَا لَحْمًا ۚ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ قَالَ أَعْلَمُ أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

“Au [hukuzingatia mfano wa] kama yule aliyepita katika kijiji nacho ni kilichoporomoka kabisa juu ya mapaa yake – akasema: “Vipi Allaah atahuisha kijiji hichi baada ya kufa kwake?” Basi Allaah alimfisha miaka mia, kisha akamfufua. Akasema: “Umekaa muda gani?” Akasema: “Nimekaa siku au sehemu ya siku”. [Allaah] akasema: “Bali umekaa miaka mia, basi kitazame chakula chako na kinywaji chako hakikuharibika na mtazame punda wako – na tutakufanya uwe ishara kwa watu – na itazame mifupa [ya punda] namna tunavyoinyanyua, kisha tunaivisha nyama.” Basi ilipombainikia alisema: “Sasa nimejua kwamba hakika Allaah juu ya kila jambo ni muweza.” (al-Baqarah 02 : 259)

4- Hekima inapelekea kufufuliwa baada ya kufa ili kila mmoja apate kulipwa kwa kile alichokichuma. Ingelikuwa si hivyo, basi ingelikuwa kuumbwa kwa watu hakuna maana, kipumbavu na pasi na hekima. Vilevile kungelikuwa hakuna tofauti yoyote kati ya mtu na mnyama katika maisha haya. Allaah (Ta´ala) amesema:

أَفَحَسِبْتُمْ أَنَّمَا خَلَقْنَاكُمْ عَبَثًا وَأَنَّكُمْ إِلَيْنَا لَا تُرْجَعُونَ فَتَعَالَى اللَّـهُ الْمَلِكُ الْحَقُّ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْكَرِيمِ

“Je, mlidhania kwamba Sisi tulikuumbeni bila kusudio na kwamba nyinyi Kwetu hamtorejeshwa? Basi ametukuka Allaah, Mfalme wa haki, hapana mungu wa haki isipokuwa Yeye! Mola wa ‘Arshi tukufu.” (al-Mu´minuun 23 : 115-116)

إِنَّ السَّاعَةَ آتِيَةٌ أَكَادُ أُخْفِيهَا لِتُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ بِمَا تَسْعَىٰ

“Hakika Saa itafika tu, nakaribia kuificha ili kila nafsi ilipwe kwa yale iliyojibidisha.” (Twaa Haa 20 : 15)

وَأَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ ۙ لَا يَبْعَثُ اللَّـهُ مَن يَمُوتُ ۚ بَلَىٰ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ لِيُبَيِّنَ لَهُمُ الَّذِي يَخْتَلِفُونَ فِيهِ وَلِيَعْلَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّهُمْ كَانُوا كَاذِبِينَ إِنَّمَا قَوْلُنَا لِشَيْءٍ إِذَا أَرَدْنَاهُ أَن نَّقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ

“Wakaapa kwa jina la Allaah nguvu ya viapo vyao kwamba Allaah hatomfufua aliyekufa. Ndio, ahadi Yake ni haki, lakini watu wengi hawajui. Ili awabainishie yale ambao wamekhitilafiana kwayo na ili wajue wale waliokufuru kwamba wao walikuwa waongo. Hakika neno Letu juu ya jambo Tunapokitaka tunakiambia: “Kuwa!” – basi kinakuwa.” (an-Nahl 16 : 38-40)

زَعَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَن لَّن يُبْعَثُوا ۚ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبْعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلْتُمْ ۚ وَذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ

“Waliokufuru wamedai kwamba kamwe hawatofufuliwa. Sema: “Bali ndio! Naapa kwa Mola wangu, bila shaka mtafufuliwa, kisha mtajulishwa kwa yale yote mliyoyatenda; na hayo kwa Allaah ni mepesi.” (at-Taghaabuun 64 : 07)

Watakapobainishiwa dalili hizi wale wenye kupinga kufufuliwa na wakaendelea kupinga, basi watakuwa ni wenye kiburi na wakaidi.

وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنقَلَبٍ يَنقَلِبُونَ

“Na hivi karibuni watakuja kujua wale waliodhulumu ni mgeuko aina gani watakaogeuka.” (ash-Shu´araa´ 26 : 227)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 145-148
  • Imechapishwa: 04/06/2020