82. Kitenguzi cha pili: mwenye kuchukia kitu alichokuja nacho Mtume

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

La tano:

Yule mwenye kuchukia kitu katika yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ijapokuwa atakifanya, amekufuru.

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ

”Hivyo kwa kuwa wao wameyachukia yale Aliyoyateremsha Allaah, basi akayaharibu matendo yao.” (Muhammad 47 : 09)

MAELEZO

Amesema Shaykh (Rahimahu Allaah):

“Yule mwenye kuchukia kitu katika yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ijapokuwa atakifanya, amekufuru. Dalili ya hilo ni maneno Yake (Ta´ala):

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ

”Hivyo kwa kuwa wao wameyachukia yale aliyoyateremsha Allaah, basi akayaharibu matendo yao.”

Bi maana akayabatilisha. Ni dalili inayofahamisha kwamba kuchukia kitu katika aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kuritadi kutoka katika Uislamu na kwamba jambo hili linayaharibu matendo ya mtu. Hilo ni kwa sababu miongoni mwa misingi ya imani na nguzo za imani ni pamoja na kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Wake, siku ya Mwisho na Qadar kheri na shari yake. Mwenye kuvunja kitu katika hayo hawi muumini. Makusudio ya maneno Yake (Ta´ala):

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ

”Hivyo kwa kuwa wao wameyachukia yale aliyoyateremsha Allaah.”

kunaingia humo Qur-aan na Sunnah vilevile aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 111
  • Imechapishwa: 19/11/2018