82. Khawaarij na Mu´tazilah ndio wanaopinga uombezi

Kuna ambao wanapinga uombezi kabisa kama Mu´tazilah na Khawaarij. Ahl-us-Sunnah ndio wako kati na kati katika mlango huu. Wanaona kuwa kuna sampuli mbili za uombezi:

1 – Uombezi uliokataliwa.

2 – Uombezi uliothibitishwa.

Sisi hatupingi uombezi moja kwa moja kama ambavyo vilevile hatuuthibitishi moja kwa moja. Ni lazima kupambanua kwa minajili ya kuoanisha baina ya Aayah katika mlango huu. Huku ndio kuwa na uelewa katika dini ya Allaah (´Azza wa Jall) na ndio njia ya wale waliobobea katika elimu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 175
  • Imechapishwa: 13/01/2024