4- Yaziyd bin Rukaan bin al-Muttwalib ameeleza: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaposimama kwa ajili ya jeneza aliswalie basi husema:

اللهم عبدك وابن أمتك احتاج إلى رحمتك، وأنت غني عن عذابه، إن كان محسنا فزد في حسناته، إن كان مسيئا فتجاوز عنه

“Ee Allaah! Mja Wako na mtoto wa kijakazi Wako ni muhitaji wa huruma Yako Nawe ni mkwasi wa kumuadhibu. Kwa hivyo akiwa ni mwema basi mzidishie katika mema yake na akiwa ni muovu msamehe.”

[Kisha aombe kile ambacho Allaah anataka kukiomba]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam-ul-Kabiyr” (22/249/247) kwa ziada. al-Haakim (01/259) ambaye amesema:

“Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh. Yaziyd bin Rukaanah na Abu Rukaanah ni Maswahabah wawili.”

adh-Dhahabiy ameafikiana naye. Pia ameipokea Ibn Qaaniy´ kama ilivo katika “al-Iswaabah”.

Inayo shahidi kupitia kwa Sa´iyd al-Maqburiy kwamba alimuuliza Abu Hurayrah:

“Ninaapa kwa jina la Allaah nitakupa khabari. Hulifuata kuanzia kwa jamaa zake, ninapowekwa basi huleta Takbiyr, kumhimidi Allaah, kumswalia Mtume wake kisha husema:

اللهم إنه عبدك وابن عبدك وابن أمتك: كان يشهد أن لا إله ألا أنت، وأن محمدا عبدك ورسولك، وأنت أعلم به، اللهم إن كان محسنا فزد في حسناته، وإن كان مسيئا فتجاوز عن سيئاته، اللهم لا تحرمنا أجرة، ولا تفتنا بعده

“Ee Allaah! Hakika huyu ni mja Wako, mtoto wa mtumwa Wako na mtoto wa kijakazi Wako alikuwa  akishuhudia ya kwamba hapana mungu wa kweli isipokuwa Wewe na kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wako na wewe ni mjuzi zaidi wa kumjua kuliko sisi. Ee Allaah! Akiwa ni mwema basi mzidishie katika mema yake na akiwa ni muovu msamehe makosa yake. Ee Allaah! Usitunyime ujira Wake na wala usitufitinishe baada ya kuondoka kwake.”

Ameipokea Maalik (01/227), Muhammad bin al-Hasan amepokea kutoka kwake (164-165), Ismaa´iyl al-Qaadhwiy katika “Fadhwl-us-Swalaatu ´alayhi (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) nambari (93), 27 kwa cheni ya wapokezi yenye kunasibishwa kwa Swahabah lakini ambayo ni Swahiyh sana. al-Haythamiy ameitaja kimlolongo kutoka kwake du´aa ambayo imerufaishwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka katika Hadiyth ya Abu Hurayrah ambaye amesema:

“Ameipokea Abu Ya´laa na wapokezi wake ni wa wapokezi wa Swahiyh.”

Imepokelewa kwa tamko lingine katika sentesi yake ya mwisho. Nayo ni aina ya pili, uk. 124.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 158-159
  • Imechapishwa: 07/02/2022