82. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa pili wa an-Nisaa´

al-´Ayyashiy amesema:

“Abu Baswiyr ameeleza kuwa Abu ´Abdillaah amesema: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye mzazi mmoja na ´Aliy mzazi wa pili.” Nikasema. “Hayo yametajwa wapi katika Kitabu cha Allaah?” Akasema: “Soma:

وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا

“Mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote. Na watendeeni wema wazazi wawili.”[1]

Abu Baswiyr ameeleza kuwa Abu Ja´far amesema kuhusu maneno ya Allaah:

وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا

“Na watendeeni wema wazazi wawili.”[2]

Maneno haya yanaufanya mwili kusisimka. Maneno hayawezi kuabiria maana yake ya utwevu pamoja na uchafu wa uzushi wake. Haki za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya Ummah ni kubwa, jambo ambalo tumeshatangulia kulitaja. Allaah amemtuma Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) awe ni rahmah kwa walimwengu. Amebainsiha haki za Allaah, haki za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), haki za waumini wao kwa wao, haki za ndugu, haki za mayatima, haki za masikini, haki za wasafiri, haki za Ahl-udh-Dhimmah mpaka haki za wanyama.

Katika Aayah hii Allaah ameamrisha kumuabudu peke yake na amekataza kumshirikisha. Kisha akawaamrisha watu watekeleze haki za wazazi wawili na kuwatendea wema. Kuna Aayah nyingi juu ya hilo ikiwa ni pamoja vilevile na zifuatazo:

وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۚ إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا

“Mola wako ameamrisha, msiabudu yeyote isipokuwa Yeye pekee. Na [ameamrisha vilevile] kuwatendea wema wazazi wawili. Kama mmoja wao akifikia uzee naye yuko pamoja nawe au wote wawili, basi usiwaambie: “Uff!” na wala usiwakemee, na zungumza nao maneno mazuri. Na wainamishie bawa la unyenyekevu kwa huruma, na waombee: “Mola wangu! Warehemu kama walivyonilea utotoni!”[3]

وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ وَهْنًا عَلَىٰ وَهْنٍ وَفِصَالُهُ فِي عَامَيْنِ أَنِ اشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ إِلَيَّ الْمَصِيرُ وَإِن جَاهَدَاكَ عَلَىٰ أَن تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۖ وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا ۖ وَاتَّبِعْ سَبِيلَ مَنْ أَنَابَ إِلَيَّ

“Tumemuusia binaadamu juu ya wazazi wake wawili. Mama yake ameibeba mimba yake [ikimzidishia] udhaifu juu ya udhaifu na [kumnyonyesha na] kumuachisha kwake ziwa katika miaka mwili ya kwamba: unishukuru Mimi na wazazi wako – Kwangu ndio marejeo ya mwisho. Lakini wakikufanyia juhudi kwamba unishirikishe na yale usiyokuwa na elimu nayo, basi usiwatii. Lakini suhubiana nao duniani kwa wema na ufuate njia ya anayerudi Kwangu.”[4]

Namna hii Raafidhwah wanakipotosha Kitabu cha Allaah na wanaziharibu hakiza viumbe wa Allaah. Bali wanaziharibu hata haki za Allaah kwa kutumia jina la ´Aliy na familia ya Mtume.

[1] 04:36

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/241).

[3] 17:23-24

[4] 31:14-15

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 124
  • Imechapishwa: 13/04/2017