81. Tatizo kubwa la leo ni suala la Haakimiyyah

Masuala ya kuhukumu kwa yale aliyoteremsha Allaah ni masuala makubwa na ndani yake kuna pambanuzi, kama walivyosema wanachuoni wa tafsiri ya Qur-aan. Asipachikwe kufuru kila yule mwenye kuhukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah. Bali inatakiwa kupambanua katika jambo hili; ikiwa mtu anaonelea hukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah ndio bora, akaona zinalingana au akaona kuwa mtu ni mwenye khiyari, huyu ndiye ambaye atahukumiwa ukafiri unaomtoa katika Uislamu. Ama yule mwenye kuona kwamba hukumu ya Allaah ndio ya lazima na ndio ya haki, lakini akaenda kinyume nayo kwa sababu ya matamanio, rushwa au pato la kidunia, huyu anahukumiwa kufuru ndogo na kwamba ni mtenda dhambi kubwa. Amesema (Ta´ala):

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ

”Yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio mafasiki.” (al-Maaidah 05:47)

Kichenguzi hichi cha nne alichotaja Shaykh (Rahimahu Allaah) ndani yake kuna masuala muhimu na hilo ndio tatizo la wakati wetu wa leo.Anatakiwa kuhukumiwa kutenda dhambi nzito na kwamba imani yake ni pungufu na kwamba ni khatari.

Tunamuomba Allaah (´Azza wa Jall) awawafikishe watawala wa waislamu wahukumu kwa yale aliyoteremsha Allaah na awawafikishe wale wanaokwenda kinyume na hayo warudi katika haki na usawa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 109-110
  • Imechapishwa: 19/11/2018