81. Kuadhini na kukimu wakati maiti anapowekwa ndani ya kaburi


Swali 81: Ni ipi hukumu ya kuadhini na kukimu karibu na kaburi la maiti anapowekwa ndani yake?

Jibu: Hapana shaka kwamba hiyo ni Bid´ah ambayo Allaah hakuteremsha dalili yoyote juu yake. Hayo hayakunakiliwa kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala kutoka kwa yeyote katika Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Kheri yote inapatikana kwa kuwafuata na kufata njia yao. Allaah (Subhaanah):

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ

“Wale waliotangulia mwanzoni ambao ni Muhaajiruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema, Allaah ameridhika nao nao wameridhika Naye.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote atakayezua katika amri yetu hii yale yasiyokuwemo basi atarudishiwa mwenyewe.”[2]

Kuna maafikiano juu ya usahihi wake.

Katika tamko jengine amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu basi atarudishiwa mwenyewe.”[3]

Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema katika Khutbah ya ijumaa:

“Amma ba´d. Hakika maongezi bora ni Kitabu cha Allaah na uongofu bora ni wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), uovu wa mambo ni yale yaliyozuliwa na kila Bidah ni upotofu.”[4]

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh).

[1] 09:100

[2] al-Bukhaariy (2697) na Muslim (1718).

[3] Muslim (1718).

[4] Muslim (867).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 57-58
  • Imechapishwa: 03/01/2022