3- Waathilah bin al-Asqaa´ amesimualia:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimswalia mtu mmoja katika waislamu nikamsikia akisema:

اللهم إن فلان ابن فلان في ذمتك وحبل جوارك، فقه فتنة القبر، وعذاب النار، وأنت أهل الوفاء والحق، فاغفر له وارحمه، إنك الغفور الرحيم

“Ee Allaah! Hakika fulani mwana wa fulani yuko katika dhimma Yako na kamba ya ujirani Wako, hivyo basi mlinde na fitina ya kaburi na adhabu ya Moto – Wewe ndiye mtekelezaji na wa haki, basi msamehe na mrehemu, kwani hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”

Ameipokea Abu Daawuud (02/68), Ibn Maajah (01/456), Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake (758), Ahmad (03/471) kwa cheni ya wapokezi wake – Allaah akitaka. Ibn-ul-Qayyim ameiorodhesha katika zile zilizohifadhiwa katika du´aa zake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na an-Nawawiy akainyamazia katika “al-Majmuu´”.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 158
  • Imechapishwa: 06/02/2022