80. Uwajibu kwa viongozi kuhukumu kwa Shari´ah na wajibu kwa wahukumiwa kuyakubali hayo

Ni wajibu kwa viongozi kuhukumu kwa yale aliyoteremsha Allaah. Haya ni miongoni mwa majukumu yao. Wawalazimishe watu hukumu ya Allaah. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا وَإِذَا حَكَمْتُم بَيْنَ النَّاسِ أَن تَحْكُمُوا بِالْعَدْلِ ۚإِنَّ اللَّـهَ نِعِمَّا يَعِظُكُم بِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ سَمِيعًا بَصِيرًا

“Hakika Allaah anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe. Namtakapohukumu baina ya watu basi mhukumu kwa uadilifu. Hakika  anayokuwaidhini nayo Allaah ni mazuri kabisa; hakika Allaah ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (an-Nisaa´ 04:58)

Aayah hii ni juu ya watawala. Kuhusu wale wanaohukumiwa ni ile Aayah inayokuja baada yake:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا

”Enyi mlioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamwamini Allaah na siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri zaidi.” (an-Nisaa´ 04:59)

Hii ni kwa wanaohukumiwa. Ni wajibu kwao kuhukumiana kwa Qur-aan na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Ni wajibu kwa watawala wahukumu baina ya watu kwa yale aliyoteremsha Allaah. Vilevile ni wajibu kwa wanaohukumiwa na wananchi wahukumiane na Shari´ah ya Allaah na wala haijuzu kwao wakahukumiana na Twaaghuut na sheria zilizotungwa na watu. Amesema (Ta´ala):

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَن يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلَالًا بَعِيدًا وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ رَأَيْتَ الْمُنَافِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودًا

”Je, huoni wale ambao wanadai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako, wanataka wahukumiane kwa twaaghuut na hali wameamrishwa wakanushe hiyo na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali. Wanapoambiwa: “Njooni katika yale aliyoyateremsha Allaah na kwa Mtume, basi utawaona wanafiki wanakugeuka kikwelikweli.” (an-Nisaa´ 04:60-61)

Sababu ya kuteremka Aayah hii, kama ambavyo inatambulika, ni kwamba kulitokea ugomvi ya mtu miongoni mwa wanafiki ambao wanadai kwamba ni waislamu na kati ya myahudi. Myahudi yule akasema kwamba waende wakahukumiwe kwa Muhammad kwa sababu alitambua kuwa Muhammad hapokei rushwa. Yule mnafiki akasema waende wakahukumiwe kwa Ka´b bin al-Ashraf ambaye alikuwa myahudi kwa sababu alitambua kuwa anapokea rushwa. Huyu anayesema hivi pamoja na kwamba anadai kuwa ni muumini. Ndipo Allaah akateremsha Aayah hii:

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَن يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلَالًا بَعِيدًا وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ رَأَيْتَ الْمُنَافِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودًا

”Je, huoni wale ambao wanadai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako, wanataka wahukumiane kwa twaaghuut na hali wameamrishwa wakanushe hiyo na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali. Wanapoambiwa: “Njooni katika yale aliyoyateremsha Allaah na kwa Mtume, basi utawaona wanafiki wanakugeuka kikwelikweli.”

Mpaka katika maneno Yake:

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ

”Basi naapa kwa Mola wako hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni hakimu katika yale wanayozozana baina yao.” (an-Nisaa´ 04:65)

Wahukumiane kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati wa uhai wake na wahukumiane yale aliyokuja nayo katika Qur-aan na Sunnah baada ya kufa kwake:

ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

“Kisha wasione katika nyoyo zao uzito wowote katika uliyohukumu na wajisalimishe kwa unyenyekevu.” (an-Nisaa´ 04:65)

Ni wajibu kwa waislamu, watawala na wale wenye kutawaliwa, wahukumu na wahukumiane kwa Shari´ah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Wasiibadili kwa kuleta kitu kingine. Watawala hawatakiwi kusema kwamba wanaziopo zile nchi kubwa na kwamba nchi hizo ndizo zimewalazimisha. Hili halijuzu. Wao ni waislamu. Ni wajibu kwao kushikamana na Uislamu. Kama inavyotambulika kanuni za kimataifa nchi hairuhusiwi kuingilia kati mambo ya siasa za kindani za nchi nyingine. Ndivi ndivo zinavosema. Kuhusu hukumu ya Allaah, basi itambulike kuwa ´hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba`. Lakini tukizitazama kanuni zao wao tunaona kuwa wanasema kwamba haijuzu kwa nchi kuingilia kati kanuni na mambo ya kindani ya nchi nyingine. Vipi basi watawala hawa watasema kuwa wamelazimishwa? Hili ni jambo lisilojuzu kabisa. Haijuzu kwa mtawala wa waislamu kuzinyenyekea hukumu zisizokuwa za Allaah (Ta´ala). Allaah (Jalla wa ´Alaa) anasema kumwambia Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ إِلَيْكَ

“Wahukumu baina yao kwa yale aliyoyateremsha Allaah na wala usifuate matamanio yao na wala usifuate matamanio yao na tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya yale aliyokuteremshia Allaah.” (al-Maaidah 05:49)

Mazungumzo haya anazungumzishwa kila mtawala ambaye anawatawala waislamu baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 107-109
  • Imechapishwa: 19/11/2018