Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Allaah (Subhaanah) ameiumba Pepo na kuifanya kuwa ni makazi ya milele juu ya vipenzi Vyake.

MAELEZO

Miongoni mwa mambo yaliyoko Aakhirah ni Pepo na Moto. Allaah ameuandaa Moto kwa ajili ya makafiri na Pepo ni kwa ajili ya wale wenye kumcha. Vimeumbwa hivi sasa. Si kwamba vitaumbwa hiyo siku ya Qiyaamah, kama wanavosema wapotofu. Vimeshaumbwa hivi sasa. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَسَارِعُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ

“Kimbilieni msamaha kutoka kwa Mola wenu na Pepo upana wake ni wa mbingu na ardhi imeandaliwa kwa wenye kumcha Allaah.”[1]

Ina maana kwamba vimeshaandaliwa na kuumbwa. Dalili nyingine ni lile joto wakati wa kiangazi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika ukali wa joto ni katika uvukizi wa Moto.”[2]

Yanafahamisha kwamba Pepo na Moto vimekwishaumbwa. Maneno yake mtunzi:

“… na kuifanya kuwa ni makazi ya milele juu ya vipenzi Vyake.”

Kama tulivosema amesema (Ta´ala):

وَسَارِعُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ

“Kimbilieni msamaha kutoka kwa Mola wenu na Pepo upana wake ni wa mbingu na ardhi imeandaliwa kwa wenye kumcha Allaah.”

[1] 3:133

[2] al-Bukhaariy (535).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 60-61
  • Imechapishwa: 17/08/2021