8. Quraysh kuwasusa Banuu Haashim na Banuul-Muttwalib

Baada ya hapo akasilimu Hamzah ami yake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wengine wengine. Uislamu ukaanza kuenea. Quraysh walipoona hivyo wakachukulia kwa ubaya na wakakusanyika kwa ajili ya kuwakata Banuu Haashim na Banuul-Muttwalib kwa njia ya kutofanya nao biashara, kutowaoza, kutowazungumzisha wala kutokaa pamoja nao mpaka wamsalimishe kwao Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wakaandika ilani na kuitundika kwenye sakafu ya Ka´bah. Inasemekana aliyeiandika ni Mansuur bin ´Ikrimah bin ´Aamir bin Haashim bin ´Abdi Manaaf. Maoni mengine yanasema kuwa ilikuwa ni an-Nadhr bin al-Haarith. Baada ya hapo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaomba dhidi yake na mkono wake ukapooza.

Banuu Haashim na Banuul-Muttwalib, waumini na makafiri kati yao, wakajiunga. Isipokuwa tu Abu Lahab ndiye ambaye aliwasapoti Quraysh na akabaki katika hali yake. Karibu miaka mitatu hakuna aliyewajia.

Kadri jinsi muda unavyoenda baadhi ya Quraysh wakataka kusitisha ilani. Ilikuwa ni Hishaam bin ´Amr bin Rabiy´ah bin al-Haarith bin Hubayyib bin Judhaymah bin Maalik bin Hisl bin ´Aamir bin Lu’ayy. Mutw´im bin ´Adiyy akakubali hilo na kundi linguine katika Quraysh wakakubali hilo. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawaeleza watu wake kuwa Allaah alituma mchwa kwenye ilani ile ikala yote yaliyo ndani yake isipokuwa jina la Allaah (´Azza wa Jall). Mambo yalikuwa namna hiyo. Kisha Banuu Haashim na Banuul-Muttwalib wakarejea Makkah. Mkataba wa amani ukafanyika kwa nguvu licha ya upindani wa Abu Jahl ´Amr bin Hishaam.

Huku na kule watu wa Abyssinia wakafikiwa na khabari kuwa Quraysh wamesilimu ambapo wengi wakarudi Makkah. Wakakuta mitihani na matatizo yako vilevile kama yalivoykuwa mwanzoni. Wakabaki Makkah mpaka walipohama kwenda al-Madiynah. Isipokuwa tu as-Sakraan bin ´Amr, mume wa Sawdah bint Zam´ah, ambaye alikufa baada tu ya kufika Makkah kutoka Abyssinia, Salamah bin Hishaam na ´Ayyaash bin Abiy Rabiy´ah ambao hawakuweza kuhama na ´Abdullaah bin Makhramah bin ´Abdil-´Uzzaa ambaye alikamatwa. Siku ya Badr alikimbia kutoka kwa washirikina na akajiunga na waislamu.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fusuwl fiy Siyrat-ir-Rasuwl, uk. 24-26
  • Imechapishwa: 18/03/2017