8. Ni ipi hukumu ya muislamu mtenda dhambi?


Swali 8: Ni ipi hukumu ya muislamu mtenda dhambi?

Jibu: Yule mwenye kuamini na ni mwenye kumuabudu Allaah peke yake na wakati huo huo ni mwenye kuendelea katika maasi, ni muumini kwa ile imani alionayo na ni mtenda dhambi kutokana na yale mambo ya wajibu alioacha.

Imani yake ni pungufu. Anastahiki kulipwa kutokana na imani yake na kuadhibiwa kutokana na madhambi yake. Pamoja na hivyo hatodumishwa Motoni.

Imani kamilifu na iliotimia inamzuia mtu na kuingia Motoni.

Imani pungufu inamzuia mtu na kudumu Motoni.

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamm-ul-Muhimmaat, uk. 46
  • Imechapishwa: 25/03/2017