8. Mwenye kutafuta utajiri basi Allaah atamtajirisha

23- Muslim amepokea kupitia kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba kuna watu wa Answaar walimuomba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawapa, wakamuomba [tena] akawapa mpaka kile alichokuwa nacho kikaisha. Akasema:

“Sintokuwa na mali nikaacha kuwapa. Mwenye kutaka utakaso basi Allaah atamtakasa. Mwenye kutafuta utajiri basi Allaah atamtajirisha. Mwenye kutaka uoni wa mbali [baswiyrah] basi Allaah atamfanya awe hivo. Hakuna aliepewa zawadi bora na ilio kuvunjufu zaidi kuliko subira.”[1]

24- Wanachuoni wetu (Rahimahumu Allaah) wamesema “Mwenye kutaka utakaso” bi maana kusubiri. Miongoni mwa hayo ni Kauli ya Allaah (Ta´ala):

وَلْيَسْتَعْفِفِ الَّذِينَ لَا يَجِدُونَ نِكَاحًا حَتَّىٰ يُغْنِيَهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ

“Na wajizuilie na uchafu wale wasiopata chakutolea, mpaka Allaah Awatajirishe kwa fadhila Zake.” (24:33)

Ibn ´Arafah na watu wengine wa lugha wamesema:

“Basi na asubiri.”

Maana yake ni kwamba yule mwenye kusubiri na kuacha kuwaomba watu kitu basi Allaah atamtakasa uso wake na kumwondoshea ufukara wake.

“Mwenye kutafuta utajiri… ” – bi maana kutoka kwa Allaah.

“… basi Allaah atamtajirisha” – bi maana atautajirisha moyo wake au atampa na kuacha kuwategemea viumbe. Inawezekana vilevile Allaah akamtukuza mtu huyo na kumpa yote mawili.

25- Ibn Abiyd-Dunyaa amepokea kuwa Bakr bin ´Abdillaah akisema katika du´aa yake:

“Ee Allaah! Turuzuku kunakofadhila Zako ambazo zitatufanya kukushukuru zaidi na kukutegemea Wewe zaidi na kutowategemea wengine wote.”

[1] al-Bukhaariy (03/335) na Muslim (02/729).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad al-Qurtwubiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Hirsw biz-Zuhd wal-Qanaa´ah, uk. 28-29
  • Imechapishwa: 18/03/2017