8. Mchumba asimtazame mwanamke faragha


Ili mtu aweze kumwangalia mwanamke ambaye anataka kumchumbia inatakiwa isiwe faragha. Dalili ya hilo ni jumla ya Hadiyth ambazo zinakataza mwanaume kuwa faragha na mwanamke ajinabi. Haifai kumwangalia ikiwa hayuko na Mahram wake. Hakuna dalili maalum juu ya hilo. Hapa kutabainika makosa yanayofanywa na watu sampuli mbili:

1- Wakati mchumba anapokuja kwa mlezi na kumkinaisha kuwa anataka kumchumbia mwanamke na hivyo akataka kumuona, mlezi anasema kuwa hawana wasichana wenye kuangaliwa.

2- Wakati mchumba anapokuja kwa mlezi na kumuomba hali kadhalika, mlezi anamwambia amchukue na aende kutembea naye, aende kula naye, kaa naye, zungumza naye, pataneni, juaneni, zisomeni tabia zenu na kila kitu. Sivyo tu, bali anamwacha akae naye faragha kwenye chumba ili waweze kuzungumza.

Hali zote hizi mbili ni zenye kulaumika. Hali ya kati na kati ni ile aliyoelekeza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mwanaume amwangalie mwanamke pasina kuwa faragha. Amwangalie wakati yuko na mlezi wake.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 15-16
  • Imechapishwa: 24/03/2017