Anasemaje muheshimiwa Shaykh Hasan al-Bannaan ambaye ameandika mwaka ulopita kwenye “Mudhakkiraat-ud-Da´wah wad-Daa´iyah” ya kwamba kutawassul kupitia mawalii ni suala ambalo [wanachuoni] wametofautiana kama maoni mengine madogo madogo ya Hanafiyyah na Shaafi´iyyah juu ya kusoma al-Faatihah na kwamba haijuzu kuwafarikanisha waislamu?

Je, haoni kuwa kwa maoni haya ya khatari yanazidi kuwaweka al-Ikhwaan mbali na dini ya kweli?

Je, haoni kuwa kwa maoni haya na kuyapitisha kwake na kuyaeneza kwenye gazeti lake linazozunguka linapelekea al-Ikhwaan wengi kuyatendea kazi katika mambo mengi ya ´Aqiydah kwa vile wanaonelea kuwa hazungumzi kwa matamanio yake?

Amejithibitishia mwenyewe jinsi wafuasi wake ni zaidi ya mamilioni. Anasemaje lau milioni ya wafuasi wake watachukua na kuhalalisha suala la Tawassul ili wajinga ´Awwaam wahakikishe kuwa ni waislamu wa kihakika?

Je, Tawassul unayoashiria wewe ni katika utukufu, nguvu na heshima ya Uislamu?

Huenda atajirudi na kutamka haki ambayo tunataraji anaiamini ndani ya moyo wake lakini hataki kuieneza ili asikose kundi lake. Ama kuhusu upupiaji wa dini ya Allaah…

Ni jambo lisilokuwa na shaka yoyote juu ya kwamba kiongozi wa kundi amehifadhi Kauli ya Allaah ambayo haiwezi kubadilishwa:

وَآمِنُوا بِمَا أَنزَلْتُ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَكُمْ وَلَا تَكُونُوا أَوَّلَ كَافِرٍ بِهِ ۖ وَلَا تَشْتَرُوا بِآيَاتِي ثَمَنًا قَلِيلًا وَإِيَّايَ فَاتَّقُونِ وَلَا تَلْبِسُوا الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُوا الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

“Na aminini yale Niliyoyateremsha yenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nanyi, na wala msiwe wa kwanza wenye kuzikanusha na wala msibadili Aayah Zangu kwa thamani ndogo na Mimi tu nicheni. Na wala msichanganye haki kwa batili na mkaficha haki ilihali mnajua.”[1]

Ni hakika pia anasoma:

إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِنَ الْكِتَابِ وَيَشْتَرُونَ بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًاۙ أُولَـٰئِكَ مَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ إِلَّا النَّارَ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّـهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

“Hakika wale wanaoficha yale aliyoyateremsha Allaah katika Kitabu na wakabadilisha kwacho kwa thamani ndogo; hao hawali katika matumbo yao isipokuwa Moto na wala Allaah hatowasemesha Siku ya Qiyaamah na wala hatowatakasa nao watapata adhabu iumizayo.”[2]

Profesa muheshimiwa! Mpwekeshe Allaah. Usisahau kuwa utaulizwa juu ya wafuasi wako ambao wanaunguwa kwa hamasa juu yako na kukutetea. Liseme mara moja tu kwa ajili ya Allaah. Usighurike na idadi hii kubwa hata kama utapendezwa na wingi mchafu:

كَم مِّن فِئَةٍ قَلِيلَةٍ غَلَبَتْ فِئَةً كَثِيرَةً بِإِذْنِ اللَّـهِ

“Makundi mangapi machache yameshinda makundi mengi kwa idhini ya Allaah?”[3]

Si wewe ndiye unasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio kiongozi wako na Qur-aan katiba yako. Je, ni katika ujumbe wa kiongozi wako kutawassul kupitia maiti walioumbuka na mawe yasiyosikia?

Je, kuna Aayah hata moja kwenye katiba yako, Qur-aan, inayokuhalalishia kuinama na kujisalimisha kwa ambaye kukudhuru kwake kuko karibu zaidi kuliko kukunufaisha?

Wewe unataka mamilioni ya wafuasi. Lakini unataka waumini wenye kujenga mnara wa Uislamu wao juu ya mchanga au namna hii tu? Wanabomoa kile kilichobaki katika dini na mikono yao tu.

Ee Shaykh! Wafunze juu ya kwamba Allaah Pekee ndiye Mola Wao na kwamba ni Mwenye nguvu na utukufu. Wafunze kurejea Kwake na kujisalimisha Kwake (Subhaanah).

Je, kuna tofauti juu ya kwamba shirki sio shirki? Je, kuna utata wowote juu ya kwamba yule mwenye kumuomba mwingine asiyekuwa Allaah ni muumini? Sikiliza nasaha kutoka kwa kijana kama mmoja katika wavulana wako:

إِنَّمَا كَانَ قَوْلَ الْمُؤْمِنِينَ إِذَا دُعُوا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ أَن يَقُولُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Hakika si venginevyo kauli ya waumini [wa kweli] wanapoitwa kwa Allaah na Mtume Wake ili Awahakumu baina yao basi husema: “Tumesikia na tumetii” – na hao ndio wenye kufaulu!”[4]

Soma Qur-aan kwa ajili ya Allaah. Fanya utafiti katika Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Aayah hii yenye kukata ushauri inatosheleza:

وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا

“Na kwamba misikiti ni [kwa ajili] ya Allaah, hivyo basi msiombe [msimuabudu] yeyote pamoja na Allaah.”[5]

Wito huu umetakasika na msafi. Huenda muheshimiwa Shaykh akaikubali na akafikisha haki ilio wazi:

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ

“Sema: “Enyi watu wa Kitabu! Njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu, kwamba tusiabudu isipokuwa Allaah pekee na wala tusimshirikishe na chochote, na wala wasichukue baadhi yetu wengine [kuwafanya] waungu badala ya Allaah.” Wakikengeuka, basi semeni: “Shuhudieni kwamba sisi ni waislamu [tunaojisalimisha kwa Allaah].”[6]

[1] 03:64

[2] 02:174

[3] 02:249

[4] 24:51

[5] 72:18

[6] 03:64

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan al-Wakiyl
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Gazeti al-Hadiy an-Nabawiy (10/1367) Lamahaat ´an Da´wat-il-Ikhwaan al-Muslimiyn, uk. 23-26
  • mkusanyaji: Muhammad bin ´Iwadhw bin ´Abdil-Ghaniy