Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Atatoka ndani yake kwa uombezi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wale watenda madhambi makubwa ambao atawaombea uombezi kutoka katika Ummah wake.

MAELEZO

Waumini watenda madhambi watatoka ndani yake, ima kutokana na fadhilah za Allaah au uombezi wa waombezi. Mwombezi mkubwa ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa ajili ya Allaah kumkirimu mwombezi na kumuonea huruma mwombewaji basi atamwacha amwombee yule Anayemtaka Yeye. Malaika, mawalii na watoto waliokufa kabla ya baleghe watafanya uombezi. Wote hawa Allaah amewapa nafasi ya kuwaombea waumini siku ya Qiyaamah. Uombezi ni kwa ajili ya wale walioingia Motoni ili watoke nje na kwa wale ambao wamestahiki kuingia Motoni ili wasiingie ndani yake. Allaah atawakubalia uombezi wao na kuwasalimisha kutokamana na Moto.

Uombezi una sharti mbili:

1 – Ni lazima uwe kwa idhini ya Allaah. Amesema (Ta´ala):

مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ

“Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake?”[1]

2 – Yule mwombewaji ni lazima awe muumini. Makafiri na washirikina hawatonufaika na uombezi wa waombezi. Amesema (Ta´ala):

مَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ حَمِيمٍ وَلَا شَفِيعٍ يُطَاعُ

”Madhalimu hawatokuwa na rafiki wa dhati na wala mwombezi anayetiiwa.”[2]

فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ

“Basi haitowafaa uombezi wowote wa waombezi.”[3]

[1] 02:255

[2] 40:18

[3] 74:48

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 60
  • Imechapishwa: 17/08/2021