79. Hukumu ya Allaah ni yenye kuenea katika kila kitu


Kuhukumu kwa yale aliyoteremsha Allaah ni jambo limeenea na sio katika mambo ya magomvi na migogoro mahakamani peke yake. Hivyo ndivo wanavyofikiria baadhi ya watu. Kuhusu mambo ya ´Aqiydah watu waachwe na kila mmoja afuate na kuchagua atakacho. Hili ni jambo kubwa na la khatari sana. Hukumu ya Allaah ni yenye kuenea katika mambo yote haya na zaidi ya hapo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 107
  • Imechapishwa: 19/11/2018