79. Du´aa ya kwanza ya kumuombea maiti


81- Aombe ndani yake zile du´aa zilizothibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Katika hizo nimesimamia nne:

1-  ´Awf bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimswalia maiti ambapo nikahifadhi kutoka katika du´aa yake akisema:

اللهم اغفر له وارحمه، وعافه واعف عنه، وأكرم نزله، ووسع مدخله، واغسله بالماء والثلج والبرد، ونقه من الخطايا كما نقيت (وفي رواية: كما ينقي) الثوب الابيض من الدنس، وأبدله دارا خيرا من داره، وأهلا خيرا من أهله، وزوجا (وفي رواية: زوجة) خيرا من زوجه، وأدخله الجنة، وأعذه من عذاب القبر، ومن عذاب النار، قال: فتمنيت أن أكون أنا ذلك الميت

“Eee Allaah! Mghufurie na mrehemu, muafu na msamehe na mtukuze kushuka kwake [kaburini] na mpanulie maingilio yake na muoshe na maji na kwa theluji na barafu na mtakase na makosa kama Ulivyoitakasa nguo (katika upokezi mwingine imekuja: “Kama inavotakaswa) nguo nyeupe kutokamana na uchafu na mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba  yake na jamaa bora kuliko jamaa zake na mume (katika upokezi mwingine imekuja: mke) bora kuliko mke wake na mwingize Pepo na mlinde na adhabu ya kaburi na adhabu ya Moto.”

Msimuliaji amesema: “Nilitamani mimi ndiye niwe huyo maiti.”

Ameipokea Muslim (03/59-60), an-Nasaa´iy (01/271), Ibn Maajah (01/4256), Ibn-ul-Jaaruud (264-265), al-Bayhaqiy (04/40), at-Twayaalisiy (999), Ahmad (06/23, 28) na mtiririko ni wa Muslim, upokezi wa pili ni wake katika moja ya upokezi, na ni wa waliosalia isipokuwa Ahmad na al-Bayhaqiy anao upokezi wa tatu.

Katika upokezi wa Ibn Maajah na at-Twayaalisiy imetajwa kwamba maiti alikuwa ni mwanamme wa ki-Answaar. Lakini katika cheni ya wapokezi wake yuko Faraja bin Fadhwaalah – naye ni mnyonge – kutoka kwa ´Iswmah bin Raashid ambaye hatambuliki.

Hadiyth ameitoa at-Tirmidhiy (02/141) mukhtasari ambaye amesema:

“Hadiyth ni geni na Swahiyh. Muhammad bin Ismaa´iyl amesema – yaani al-Bukhaariy –Hadiyth ambayo ni Swahiyh zaidi kuhusiana na maudhui haya ni hii.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 157
  • Imechapishwa: 06/02/2022