78. Viumbe wote ni wajibu kumfuata Mtume Muhammad (صلى الله عليه وسلم)

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Hii ndio Dini yake. Hakuna kheri yoyote isipokuwa amewaonyesha nayo Ummah wake, na hakuna shari yoyote isipokuwa amewatahadharisha nayo. Kheri kubwa aliyowaonyesha nayo ni Tawhiyd na kila anachokipenda Allaah na kukiridhia. Na shari kubwa aliyowatahadharisha nayo ni shirki na kila anachokichukia Allaah na kukibughudhi.

MAELEZO

Allaah amemtuma kwa watu wote na Allaah akafaradhisha kwa viumbe wote – majini na watu – kumtii. Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا

“Sema: “Hakika mimi ni Mtume wa Allaah kwenu nyinyi nyote.” (al-A´raaf 07 : 158)

Allaah amemtuma kwa watu wote – Bi maana Allaah amemtumiliza kwa watu wote.

Sema: “Hakika mimi ni Mtume wa Allaah…  – Hii ni dalili inayoonyesha kwamba Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametumilizwa na Allaah kwa watu wote na kwamba aliyemtuma ni Yule ambaye ndiye Mfalme wa mbingu na ardhi. Yule ambaye mikononi mwake ndio mna kuhuisha na kufisha. Yeye pekee (Subhaanah) ndiye mwenye haki ya kupwekeshwa kwa kuabudiwa kama ambavyo anavyopwekeshwa katika uola Wake. Mwishoni mwa Aayah akatuamrisha (Subhaanahu wa Ta´ala) kumuamini na kumfuata Mtume huyu asiyekuwa msomi. Kufanya hivo ndio sababu ya uongofu wa kielimu na utendakazi, nao ni uongofu wa kuelekeza njia ya sawa na uongofu unaomuwafikisha mtu kuweza kuifuata. Yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Mtume kwa majini na watu wote.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 141-142
  • Imechapishwa: 03/06/2020