77. Ni lazima kwa kila muislamu kukitilia umuhimu kitabu hiki

Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Allaah ndiye anajua zaidi na swalah na amani zimwendee bwana wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahaabah zake.

MAELEZO

Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amekimalizia kitabu hiki kwa kusema:

”Allaah ndiye mjuzi zaidi.”

Namna hii ndivo mtu anatakiwa kuiegemeza elimu kwa Allaah.

Mwishoni mwa kitabu hiki nahimiza kukitilia umuhimu. Kwani kinahusiana na jambo kubwa; nguzo miongoni mwa nguzo za Uislamu ambayo ni swalah. Swalah ndio nguzo ya dini. Ni lazima kwa muislamu kupupia kujifunza sharti, nguzo na mambo ya wajibu ya swalah. Vilevile apupie kuwafunza wengine. Kwa sababu swalah haisihi isipokuwa kwa kuyatekeleza mambo hayo.

Swalah na amani zimwendee bwana wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahaabah zake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 111
  • Imechapishwa: 06/07/2022