78. Maiti anatakiwa kuelekezwa Qiblah


Swali 78: Kumwelekeza maiti Qiblah ni katika Sunnah au ni katika mambo yaliyopendekezwa tu[1]?

Jibu: Ni miongoni mwa mambo yaliyowekwa katika Shari´ah kutokana na Hadiyth isemayo:

“Ka´bah ni Qiblah chenu mliohai na wafu.”[2]

Atalazwa upande wake wa kulia na huku uso wake umeelekezwa Qiblah.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/192).

[2] Abu Daawuud (2874) kwa tamko lisemalo:

”Nyumba Tukufu ni Ka´bah ni Qiblah chenu mliohai na wafu.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 56
  • Imechapishwa: 01/01/2022